MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE

Kuku hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo mengine yanatibika kwa dawa na mengine hayana tiba, ila  pia kuku hupewa chanjo maalumu ambayo huzuia magonjwa hayo. Leo nitawaeleza baadhi ya magonjwa ambayo hushambulia kuku mara kwa mara na ambayo ni chanzo cha kuwakatisha tamaa wafugaji wa kuku.


Tuanze kwa kuangalia magonjwa yaonayohitaji chanjo ambayo ni 

1.  GUMBORO
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
      
Dalili za ugonjwa
    -Kuku kuzubaa na kulundikana, pamoja na kusinzia
    -Kuku kuharisha
    -Kuwa na vifo vingi kwa kuku

Tiba.

 Ugonjwa huu hauna tiba,,Kuku wakipewa Dawa za oxytetracycline hupunguza vifo.


Kinga  
wakinge kuku wapo kwa kuwapa chanjo ya gumboro (Gumboro vaccine)


2.  MAHEPE (Marecks)
             Ugonjwa huu husababishwa na virusi


Dalili za ugonjwa.
     -Kuku hupata ulemavu na vifo vya mara kwa mara.
   
 Tiba za ugonjwa huu.

 Ugonjwa huu hauna tiba


Kinga za ugonjwa huu.
Chanjo hutolewa kwa vifaranga wenye umri wa siku moja,vifaranga hupewa chanjo ya mahepe (Marecks vaccine)


3. NDUI YA KUKU (Fowl Pox)
            Ugonjwa huu husababishwa na virusi.


Dalili za ugonjwa huu ni;
    -Kuku hupatwa na vidonda kichwani.
    -Kuku hupata uvimbe mweupe kwenye mdomo na kushindwa kula.


Tiba za ugonjwa ndui
 Ugonjwa huu hauna tiba.


Kinga za ugonjwa huu.
Chanja kuku wako wa siku 60-90 kwa chanjo ya Ndui ya kuku (Fowl pox vaccine).

 4. MDONDO
   Ugonjwa huu husababishwa na virusi
  
Dalili za ugonjwa wa mdodndo
  -Ugonjwa huu hutokea kwa ghafla na kuenea kwa haraka
  -Vifo vya kuku huwa vingi
  -kuku hupumua kwa  shida
  -Kuku hupooza na kulemaa miguu
  -Kuku hupinda shingo yake
  -Kuku hupunguza kutaga mayai
  -kuku huarisha
  -Kuku Kuzunguka zunguka na kutembea kinyume nyume.


Tiba za ugonjwa za mdondo
Hauna tiba

Kinga za ugonjwa wa mdondo.
Chanja vifaranga wako na kuku wako kwa chanjo ya Mdondo (New castle vaccine) na urudie chanjo hii kila baada ya miezi mitatu.



Somo litaendelea siku ya kesho……..

1 Comments