USIKUBALI KUTAPELIWA KWA KUNUNUA VIFARANGA VYA UZAO WA PILI AU WATATU

Leo ningependa kuzungumzia Hii biashara ya kuku inayofanywa na baadhi ya wafugaji ambao mwisho wa siku wanazalisha vifaranga na kuwauzia wajasiliamali wengine...

Somo hili ni mahususi kwa wale wajasiliamali ambao wanakimbilia kununua vifaranga kwa watu hapa na walenga wale wanaofuga Kuroiler ama Sasso...

Kwa ufupi ni kwamba mmachezewa mchezo mchafu na baadhi ya wafugaji kwa kuwauzia vifaranga ambao ni kizazi cha pili ama tatu ambapo kuku hao perforamance yao iko chini mno tofouti na mnavyoaminishwa na hao wafugaji, mbaya zaidi wameenda mbali sana kuwauzia kwa gharama ya juu zaidi ambapo kihali inakuwa si sawa.

Labda nigusie kidogo hapa, Hawa kuku wazazi wa either Layers, Broiler ama Kuroiler/Sasso ni gharama sana kuwaingiza hapa nchini na pia uleaji wake unahitaji umakini mkubwa sana tofouti na hawa kuku wetu wa kawaida. Kwa makadrio tu kifaranga kimoja cha parent stock mpaka kuingia nchini kitakugharimu kati ya USD 15~20 hivyo ni ngumu kwa mtu wa kawaida kumudu gharama yake hivyo kupelekea makampuni makubwa kama silverlands, interchicks na mkuza chicks kuwa na kuku hao.

Baada ya kulelewa vyema kuku hao wazazi hutaga mayai na kupelekwa hatchery ambapo mayai ya broiler yatoa vifaranga vya kuku wa nyama ambavyo mtauziwa kwa lengo la kutoa nyama tu, mayai ya kuku wa mayai yatatoa kuku wa mayai kwa ajili ya mayai tu na mayai ya kuroiler/sasso vifaranga ambao watatumika kama kuku wa nyama au kwa ajili ya mayai pekee.

Sasa baadhi ya wafugaji hutumia mwanya huu kuwakuza hao kuku chotara na kupata mayai yao ambapo huyapeleka hatchery kutotoleshwa na kupata kizazi cha pili (2nd generation) na wao pia kuwauzia wafugaji wengine. Labda niwaambie tu hapa ndio huwa mnaibiwa maana performance ya kuku hao itakuwa chini sana kwa maana kwamba kuanzia utagaji, ukuaji utakuwa chini na pia kuku hawa hawatokaukiwa na magonjwa maana kinga yao ya mwili iko chini mno.

Mwisho: Kwa wafugaji ambao wangependa kuingia katika industry hii ningependa kuwataadharisha muache mara moja kununua vifaranga kwa wafugaji wa nyumbani maana mnatapeliwa mchana kweupe kwa kununua kuku ambao hawatokupa matokeo mazuri.

Kwa maana hiyo ningependa mnunue kuku hao katika makampuni makubwa ambayo yana Kuku wazazi (parent stock) mtapata matokeo mazuri tofouti na hao wa mtaani.

Maelezo yote nimefupisha katika mchoro hapo chini.

Kama kuna sehemu hujaelewa na utahitaji maelezo zaidi weka swali lako hapo Katika sanduku la maoni nami nitakujibu. 


0 Comments