KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO.

Viazi mviringo au Viazi Ulaya ni zao ambalo la asili, pia  zao hili ni miongini mwa mazao jamii ya mzizi (tuberous crop) na linalodumu, kwa jina la kitalaam linaitwa Solanum tuberosum .
Neno “Kiazi” linatokana na maana ya mmea ambao una aina “tuber ” yaani chenyewe. Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zinazoendelea. Viazi hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano. Viazi mviringo vina virutubisho vingi mfano vitamin, protin,madini na maji.

Asili yake.
Viazi mviringo kwa mara ya kwanza viligundulika huko kusini mwa nchi ya Peru na kufuatiwa kaskazini magharibi mwa nchi ya Bolivia kati ya miaka 8000 na 5000 kabla Yesu hajazaliwa (BC). Na vimekuwa viki sambaa kwa kasi katika maeneo tofauti duniani na kuwa zao la chakula katika nchi nyingi. Hapa Tanzania viazi mviringo kuzalizwa katika maeneo yenye miinuko ya kaskazini kama vile Arusha, Moshi, Lushoto na meneo ya kusini yenye miinuko kama vile mkoa wa Njombe, Iringa, Mbeya na mkoa wa Songwe. Pia maeneo ya Morogoro yenye miiunuko hususani Tarafa ya Mgeta yameonekana kuweza kuzalisha zao hili kwa wingi.


Aina za viazi.
Viazi mviringo vipo aina mbalimbali zilizoingizwa Afrika Mashariki kutoka Ulaya ambako huzalishwa kwa wingi.


Aina hizo ni kama ifuatavyo:
1. Dutch Robijn – kutoka Holland
•inavumilia kidogo ugonjwa wa ukungu
• hushambuliwa sana na Mnyauko Bakteria
• hupendwa na walaji wengi.
Roslin – kutoka Scotlland
•ngozi yake ni nyeupe
•dani ni nyeupe
• huvumulia ugonjwa wa ukungu.
Kerr’s Pink –
•ngozi yake ni nyeupe au nyekundu
•ndani ni nyeupe
•hushambuliwa sana na ukungu na Mnyauko Bakteria.


2. Atzimba – kutoka Mexico
Huvumilia ugonjwa wa ukungu
Uyole: Kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo uyole kuna aina kama baraka, sasamua, tana, subira(EAI 2329), Bulongwa, kikondo(CIP 720050).


Hali ya hewa ifaayo kwa kilimo cha viazi.
Viazi Mviringo hustawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita 1300 hadi 2700 juu ya usawa wa bahari. Viazi huhitaji mvua za kiasi cha sentimita 25 kwa wiki ambazo hutakiwa kuendela kwa muda wa miezi 3 .5 hii huweza kukuza viazi na kupata mavuno mazuri, pia hutoa mavuno mengi kwenye udongo usio mzina na unaopitisha maji kiurahisi, na uwe na rutuba.


Utayarishaji wa shamba.
Shamba linatakiwa kuandaliwa vituta vidogo vidogo kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka tuta hadi tuta, hii husaidia kuhifadhi udongo na maji na hutoa nafasi nzuri wakati wa upanukaji wa viazi. Inashauriwa pia kama matuta hayajatumika basi ni muhimu kujaza udongo kwenye shina kwani pingili za chini kwenye shina ni lazima zifunikwe na udongo ili zitoe viazi kwa wingi na hivyo mavuno huongezeka.


Utayarishaji wa mbegu.
Tumia viazi vyenye umbile dogo kama mbegu, hutakiwa kuwa na upana wa yai au upana wa sentimita 3 – 6. Kiasi cha robo tatu za tani huhitajika kuotesha ekari 1 sawa na tani 1.85 kwa hekta 1. Mbegu hazitakiwi kuhifadhiwa kwenye giza nene kwani zitaanza kutoa vichipukizi virefu vyeupe.


Sifa za mbegu bora za viazi.
1.Zenye kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja.

2. Ziwe zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi zaidi ya manne.
3. Zisiwe na wadudu pamoja na magonjwa.
4. Zitoke katika aina ambayo haishambuliwi na magonjwa kama vile ukungu na mnyauko.
4. Zenye ukubwa wa wastani unaolingana na ukubwa wa yai la kuku.

Upandaji.
Viazi hupandwa kipindi mvua zinapotaka kuanza, kuchelewa kuotesha kutapunguza kipindi cha ukuaji wa ile mizizi ili iwe viazi na hivyo kukabiliwa na kipindi cha ukavu. Uoteshaji hufanyika kwa mikono na mbegu ziwekwe chini udongo kwa kina cha sentimita 10.

Kama mbegu zitaoteshwa bila matuta basi zioteshwe kwa kina cha sentimita 15 na kufunikwa na udongo mchache na wakati wa palizi udongo utaongezwa ili kuongeza utoaji wa viazi kwa wingi. Nafasi ya kuotesha ni sentimita 75 toka mstari hadi mstari na sentimita 23 – 30kwa mche hadi mche.

Mbolea.
Kama kuna uwezo wa kupata mbolea ya asili (samadi au mboji) ni vema kutumia. Mbolea za viwandani zinazotakiwa ni zile zenye Nitrogeni kwa kiasi cha kilo 22 – 45 kwa ekari; zenye Chokaa P2O5 kwakilo 45 – 65 kwa ekari. kwa mbolea za viwandani tumia kilo 300 au mifuko 6 za mbolea ya TSP kwa hekta moja, na kilo 300 mifuko 6 za mbolea ya CAN au kilo 400 mifuko 8 ya S/A au kilo 175 mifuko 3.5 za UREA.


Upaliliaji na unyevunyevu.
Zao la viazi likioteshwa kwa nafasi zilizoshauriwa basi huweza kufunika ardhi yote na hivyo kugandamiza magugu, hii husaidia kwa kipindi cha wiki 6 za mwanzo. Katika mpando wa matuta, basi huwa ni kuondoa magugu na kujaza udongo kwenye mashina.Palilia viazi wiki mbili au tatu baada ya kuchomoza. Inulia udongo kufanya tuta zuri ili pawepo na unyevu wa kutosha na kufunika viazi kutokana na mwanga wa jua.


Maginjwa ,Wadufu & Magonjwa 
Ukungu
Ili kuzuia ugonjwa wa ukungu tumia Ridomil, changanya gram 100 za dawa katika lita 20 za maji na nyunyuzia mara baada kila wiki mbili au tatu kutegemea na hali ya hewa.

Nyunyuzia dawa ya karate kiasi cha mililita 20 mpaka 40 za dawa katika lita 20 za maji ili kuzuia wadudu kama inzi weupe na wengine. Tumia mbinu bora za kilimo kama usafi wa shamba au kilimo mzunguko kama mbinu ya kuzuia magonjwa na wadudu.
Wadudu
Vidukari:-Ni wadudu wadogo wanoshambilia majani na mashina kwa:
1. kufyonza utomvu na kusababisha kunyauka kwa mmea.
2. Majani kujikunja kuelekea juu.
3. Majani kuwa magumu
4. Mimea kudumaa
5. Pia hubeba vimelea aina ya virusi ambao huathiri mimea.
6. Pia hueneza ugonjwa wa virus.

Kuzuia: – Wakati wa utunzaji wa mbegu za viazi ni muhimu kupiga dawa ya wadudu ili kuepuka kupuliza shambani kwani dawa nyingi itapotea.
Nondo wa viazi: 
Wadudu huathiri viazi vilivyooteshwa wakati ambao sio wa msimu wa viazi. Viwavi wanaoanguliwa huingia ndani ya viazi na kusababisha kuoza. Pia huingia ndani ya viazi wakati vikiwa stoo.

Kuzuia: Otesha viazi katika kinachoshauriwa au zaidi ya sentimita 3 kwani kiwavi aingiae ndani ya hawezi kuchimba kina kirefu na inulia matuta wakati viazi vinakuwa, hii husaidia kuzuia nondo kutaga mayai.
Minyoo fundoo.
Hushambulia viazi vilivyoachwa kwa muda mrefu ardhini na kwenye ardhi iliyoathirika na mmomonyoko.

Kuzuia.

1.Usioteshe mbegu ambazo zimeshambuliwa na wadudu.
2. Andaa shamba mapema ili masalia yote ya mazao yaweze kuoza ili kutoruhusu makazi ya minyoo fundo.


Mbawakavu: -Ni wadudu wadogo ambao hutafuna majani na kuacha matundu matundu.
Kuzuia: Tumia dawa aina ya Malathion, Thiodan.


Uvunaji.
Viazi huwa tayari kuvunwa baada ya miezi 3 hadi 5 kutoka kupanda. mda wa kuvuna unategemea na mda wa kupanda na dhumuni la zao. Uvunaji wa viazi hufanyika kwa kutumia jembe la mkono, viazi vikishang’olewa kutoka chini ya udongo visiachwe kwa muda mrefu kwani vitabadilika rangi na kuwa kijani.


Ili kuifanya ngozi ya viazi kuwa ngumu na isiharibike kirahisi basi mashina yote yanyofolewe wiki 2 – 3 kabla ya kuvuta viazi juu ya udongo. Baada ya viazi kuvunwa haviwezi kuhifadhiwa kwa muda mrefu kwani huanza kuchipua.

Viazi huweza kuhifadhiwa kwenye ardhi, lakini si zaidi ya wiki 6 kwani vitakabiliwa na magonjwa na kushambuliwa na minyoo fundo. Kuvitunza viazi ardhini utahitajika kuvifunikia na nyasi ili visibadili rangi ya ngozi kwa kupigwa na jua, usiache viazi shambani bila kufunika kwa nyasi au udongo kwa mda mrefu.

Uhifadhi
Viazi vya chakula viiafadhiwe kwenye ghara hewa ya kutosha pasiwe na unyevunyevu na joto kali, Viazi vilivyowekwa ghalani visilundikwe kwa kina kirefu, visambazwe ili visipate joto.


Asante sana kwa kusoma makala haya, nikutakie siku njema na kazi njema.

14 Comments

  1. Je ni mbolea ipi ya viwandani ina faa kwa ajili ya zao hili? Na pia viki pandwa kitaalamu hekari 1 huweza kutoa kiasi gani cha mavuno?

    ReplyDelete
  2. Je ni mbolea ipi ya viwandani ina faa kwa ajili ya zao hili? Na pia viki pandwa kitaalamu hekari 1 huweza kutoa kiasi gani cha mavuno?

    ReplyDelete
  3. asante sana kwa somo lako zuri. je kwa wale tunaoishi mikoa ya kanda ya ziwa Victoria tunaruhusiwa kulima kwa udongo upi? mfano mimi ni mkulima wa mahindi niko IPILILO MASWA natamani zao hili la viazi ninaruhusiwa kulima?

    ReplyDelete
  4. hujatuambia hekari moja unaweza vuna gunia ngapi?

    ReplyDelete
  5. Asante Sana na somo zuri la viazi ulaya ...nilikua nataka kujua kwa sisi tunao ishi wilaya ya kibiti aridhi yake inakubali kuotesha viazi .?

    ReplyDelete
  6. Msaana nataka kuanza kilimo cha viazi nahitaji kujua mchanganuo mzima mfano:Hekar 1: kukodi shingapi,mbegu shingapi,madawa shingapi na nikivuna wastani wakupata shingapi?

    ReplyDelete
  7. Thank you for the class actualy new to this advrnture. From sea life to a potato farmer.my shamba has various plant few have flowers some short and brownish orthes are germinating and few are rotten.
    Well is it good to replace the rotten ones?

    ReplyDelete
  8. Thank you for the class actualy new to this advrnture. From sea life to a potato farmer.my shamba has various plant few have flowers some short and brownish orthes are germinating and few are rotten.
    Well is it good to replace the rotten ones?

    ReplyDelete
  9. Thank you for the class actualy new to this advrnture. From sea life to a potato farmer.my shamba has various plant few have flowers some short and brownish orthes are germinating and few are rotten.
    Well is it good to replace the rotten ones?

    ReplyDelete
  10. Ni zao zuri la chakula .. asanteh Kwa elimu

    ReplyDelete
  11. Vipi ukikata kata viazi vipande haviwezi kutumika km mbegu?

    ReplyDelete