MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU KABLA YA KUANZA KUFUGA NJIWA

 Ukiachana tofauti ya bei ya njiwa huanzia elfu 10 pair moja ya njiwa Wa kawaida, elfu 60 kwa wale weupe, na wengine wapo wanauzwa hadi laki 8 kwa pair moja!



(Kazi moja ya njiwa ni urembo,burudani,kitowewo na baraka)


Kabla ya kufuga njiwa hao ni vyema sasa kutambua masharti yao;

Kwanza kabisa njiwa ukiwanunua kutoka kwa mtu, sharti wawe wawili pair (dume na jike)

Kama muuzaji aliwafuga kwa banda la juu, hakikisha unakowapeleka uwaandalia banda la juu, ukiwaweka banda la chini wanaondoka

Kama banda lako la chini, tafuta muuzaji mwenye banda la chini ndipo ununue vinginevyo unashauriwa uwanyonyoe manyoya na kuwafungia siku 40 kabla ya kuwafungulia.

Njiwa wakiwa mbele yako usipende kuwajadili, hawapendi masimango wataondoka!

Ukifuga njiwa nao hufatilia nyendo zako, ukiwa mlevi hawakai wanaondoka kwasababu inasemekana kuwa njiwa wanaamini mlevi anaweza sahau kuwafungulia bandani siku moja

Njiwa wana nguvu kiimani, hawapendi mfugaji awe m-mbeya kugombana na majirani, kwasababu wakati Wa ugomvi njiwa hukaa juu ya paa wakisikiliza halafu huondoka na hawarudi tena

Njiwa hawapendi kuona Umemchinja njiwa mwenzao mbele yao, wakiona wanahama wote kwasababu wanahisi utawachinja.

Njiwa hawapendi Makelele ya kushtukiza kama honi Kali, kuwarushia jiwe na miziki mikubwa, ukifanya hivyo wanahama

Njiwa akifa mmoja, huomboleza, unashauriwa umtafutie mwenza haraka kwa njiwa anaebaki la sivyo wanaondoka

Hakikisha njiwa huwachanganyiki na kuku mwenye vifaranga, wakipararuliwa huondoka mazima.

Njiwa wanaofugwa banda la uani/nyuma/jikoni huzaliana haraka zaidi kwasababu ya mazingira tulivu

Hakikisha pakashume hawazoei kufika nyumbani kwako! njiwa hawapatani na paka pori la sivyo wanahama wote!

Inasemekana njiwa ni Wa pili kwa wivu baada ya nyegele! Hakikisha unafuga wawiliwawili.

Hayo ni machache tu kati ya masharti ya njiwa!!! je ni jambo gani unalolifahamu kuhusu njiwa tuandikie hapo kwenye maoni.

0 Comments